Visiwa vya Aland
Visiwa vya Aland (kwa Kiswidi: Åland; kwa Kifini: Ahvenanmaa) ni funguvisiwa la Bahari ya Baltiki upande wa kusini magharibi wa Ufini.
Mji mkuu ni Mariehamn kwenye kisiwa cha Fasta Åland.
Ndani ya Ufini ni jimbo lenye utamaduni wa Kiswidi lililo na hali ya pekee kikatiba na kiwango kikubwa cha kujitawala.
Funguvisiwa lina visiwa zaidi ya 6,000: vingi ni vidogo sana na 60 pekee vina watu. Jumla ya wakazi ni 26,530.
Umbali na Ufini ni kilomita 15 na Uswidi ni km 40.
Kisiwa kikubwa ni Fasta Åland upande wa magharibi. Eeno la visiwa vyote ni km² 1,554.
Historia
haririTangu mwaka 1000 BK visiwa vilikuwa chini ya Uswidi. Wakati wa Uswidi kutawala Ufini vilihesabiwa pamoja na jimbo la Kifini la Uswidi.
Tangu mwaka 1809 vilihamishwa chini ya Urusi pamoja na Ufini wote.
Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kulitokea uhuru wa Ufini pamoja na fitina kama visiwa vitakuwa sehemu ya Ufini au ya Uswidi.
Shirikisho la Mataifa liliamua mwaka 1920 ya kuwa
- visiwa vitabaki sehemu ya Ufini
- wakazi wawe na uhuru wa kutumia lugha yao ya Kiswidi na kutunza utamaduni wao
- visiwa viwe eneo bila wanajeshi
Ufini ilitekeleza azimio hili kwa sheria mbalimbali. Hivyo Aland ni sehemu ya Ufini ambako lugha rasmi pekee si Kifini bali Kiswidi. Wafini kutoka bara hawaruhusiwi kununua ardhi au nyumba moja kwa moja kama hawajaishi visiwani kwa miaka kadhaa kwanza.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Aland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ufini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Aland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |