Albano wa Mainz (jina la awali Remoundos Michail; Naxos, Ugiriki[1] - Hanum, Mainz, Ujerumani 406 hivi) alikuwa padri, mmisionari na hatimaye mfiadini.

Mt. Albano wa Mainz.

Maisha hariri

Rabanus Maurus aliandika kuwa Albano alitumwa na Ambrosi wa Milano huko Gallia kama mmisionari.

Huko Mainz, Albano alimsaidia askofu Aureus wa Mainz kujirudishia jimbo lake. Lakini mwaka 406, Wavandali walipovuka mto Rhine, Aureus alichinjwa na Albano alikatwa kichwa huku akisali.

Mara nyingine Albano huyo anachanganywa na somo wake Albano wa Uingereza, na askofu wake anachanganywa na mwingine.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Patron Saints Index: Saint Alban of Mainz". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-15. Iliwekwa mnamo 2017-06-05. 

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.