Alexander Stephanovich Popov
Alexander Stephanovich Popov (16 Machi [O.S. 4 Machi] 1859 - 13 Januari [O.S. 31 Desemba 1905] 1906) alikuwa mwanafizikia wa Urusi ambaye kwa mara ya kwanza alionyesha jinsi ya kutumia mawimbi ya umeme (redio), ingawa hakuomba leseni ya uvumbuzi wake.
Kazi ya Popov kama mwalimu katika shule ya wanajeshi wa majini wa Kirusi ilimwongoza kuchunguza matukio ya juu ya umeme.
Maisha ya awali
haririAlizaliwa na padri wa Kiorthodoksi katika mji wa Krasnoturinsk, Oblast Sverdlovsk. Alipata nia ya sayansi ya asili wakati alipokuwa mtoto. Baba yake alitaka Alexander ajiunge na ukasisi na kumpeleka kwenye shule ya seminari huko Yekaterinburg. Hapo alijenga maslahi ya sayansi na hisabati na badala ya kwenda chuo cha Theolojia mwaka 1877 alijiunga na chuo kikuu cha St. Petersburg ambako alisoma fizikia.
Baada ya kuhitimu kwa heshima mwaka 1882, alikaa kama msaidizi wa maabara katika chuo kikuu. Hata hivyo mshahara haukuwa na uwezo wa kuunga mkono familia yake, na mwaka 1883 alipata nafasi kama mwalimu na mkuu wa maabara katika shule ya Torpedo ya mafunzo ya majini ya huko Urusi.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alexander Stephanovich Popov kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |