Amatori wa Auxerre

Amatori wa Auxerre (kwa Kifaransa: Amadour au Amatre; alifariki Auxerre, leo nchini Ufaransa, 1 Mei 418) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 388 hadi kifo chake.

Sanamu yake huko Kervignac.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 1 Mei[1][2].

Maisha

hariri

Amatori alisoma teolojia chini ya Valeriani wa Auxerre, lakini wazazi walimshinikiza kuoa. Hata hivyo alikubaliana na mke wake kuishi kama kaka na dada.

Baadaye mkewe alijiunga na umonaki, naye alijiunga na kleri[3] na hatimaye akawa askofu kwa miaka 30 akijitahidi kung'oa ushirikina na kueneza heshima kwa wafiadini[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.