Anastasi wa Cluny, O.S.B. (Venezia, Italia, karne ya 11; Pamiers, leo nchini Ufaransa, 1085), alikuwa msomi ambaye alijiunga na monasteri ya Mont-Saint-Michel (Ufaransa), halafu akaishi kama mkaapweke katika kisiwa cha jirani, hadi Hugo wa Cluny alipomtembelea na kumvutia ajiunge na Wabenedikto wa Cluny. Hata hivyo mara nyingine alirudi kuishi upwekeni [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Oktoba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/93044
  2. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.