Hugo wa Cluny (pia: Hugo Mkuu au wa Semur; Semur-en-Brionnais, Ufaransa, 13 Mei 1024Cluny, 28 Aprili 1109) alikuwa abati wa 4 wa monasteri ya Kibenedikto ya Cluny kwa miaka 61, kuanzia mwaka 1049 hadi kifo chake.

Mchoro mdogo wa Mt. Hugo, kaizari Henri IV na Matilda wa Toscana.

Ni kati ya viongozi muhimu zaidi wa maisha ya kitawa katika Karne za Kati, maarufu kwa sala na huruma kwa wahitaji. Alidumisha nidhamu na kueneza Kanisa[1].

Anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Kalisti II tarehe 6 Januari 1120.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Aprili[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.