Andeoli (alifariki Bergoiata, Viviers, 208) alikuwa Mkristo kutoka Smirna (leo nchini Uturuki) aliyefanua umisionari huko Galia (leo Ufaransa) hadi alipouawa wakati wa dhuluma ya kaisari Septimius Severus.

Ngao ya Saint-Andéol-de-Clerguemort, ikimuonyesha Mt. Andeoli.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 1 Mei[1].

Maisha hariri

Andeoli alizaliwa Smirna katika karne ya 2. Akiwa shemasi, alitumwa na askofu Polikarpo,[2] kuinjilisha Galia Kusini pamoja na Benignus.

Kati ya waliowaongoa, mmojawao ni Sinforiani wa Autun, baadaye mfiadini.

Andeoli aliendelea hadi Vivarais alipouawa kwa upanga.[3]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.