Polikarpo Mtakatifu

Polikarp Mtakatifu

Mtakatifu Polikarpo (takriban 69-155) alikuwa askofu katika mkoa wa Asia (Uturuki wa leo).

Ametambuliwa kuwa mtakatifu kama mfiadini.

Sikukuu yake ni 23 Februari.

MaishaEdit

Polikarpo alikuwa mwanafunzi wa mtume Yohane na askofu wa mji wa Smirna (leo Izmir nchini Uturuki). Pengine barua kwa malaika wa Kanisa la Smirna inayopatikana katika Kitabu cha Ufunuo ilimlenga na kumsifu yeye.

Alikuwa rafiki ya Mt. Ignasi wa Antiokia ambaye alimuandikia barua maarufu.

Alikwenda Roma, Italia, kuzungumza na Mt. Papa Anicetus kuhusu maadhimisho ya Pasaka.

Mwaka 155 aliifia dini yake kwa kuchomwa moto katika uwanja wa michezo. Habari za kifodini hicho zinasifiwa kwa uzuri wake.

Sala yake wakati wa kufia diniEdit

Ee Bwana, Mwenyezi Mungu, Baba wa Mwanao mpenzi na mbarikiwa Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake tumekufahamu; Mungu wa malaika na wa wenye uwezo, wa kila kiumbe na wa kizazi chote cha waadilifu wanaoishi mbele yako: mimi nakubariki kwa kuwa siku hii na saa hii umenijalia nishiriki kikombe cha Kristo wako pamoja na wafiadini wote, kwa ufufuo wa roho na wa mwili katika uzima wa milele, katika hali ya kutoharibika kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Niweze leo kupokewa pamoja nao mbele yako kama sadaka nono na ya kupendeza, kama vile wewe, Mungu usiye na hila na msemakweli, ulivyoiandaa ukanionyesha mapema na sasa umeitimiza.

Kwa sababu hiyo na kwa mambo yote mimi nakusifu, nakuhimidi, nakutukuza pamoja na kuhani wa milele na wa kimbingu Yesu Kristo, Mwanao mpenzi, ambaye kwa njia yake kwako na kwa Roho Mtakatifu uwe utukufu sasa na nyakati zijazo. Amina.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1295
  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Polikarpo Mtakatifu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.