Ansgar Mtakatifu

Ansgarius predikar Christna läran i Sverige by Hugo Hamilton.jpg

Mtakatifu Ansgar (labda 8 Septemba 8013 Februari 865) alikuwa askofu kutoka Ufaransa.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni 3 Februari.

MaishaEdit

Ansgar alizaliwa Amiens (Ufaransa) mwanzoni mwa karne ya 9.

Alisoma katika monasteri huko Corbie.

Mwaka 826 alienda kuhubiri Injili nchini Denmark, ambako hakufanikisha sana, hivyo akaenda Uswidi.

Aliteuliwa kuwa Askofu wa Hamburg, upande wa kaskazini wa Ujerumani. Pia alikuwa balozi wa Papa Gregori IV katika Denmark na Uswidi.

Alivumilia magumu mengi sana katika kazi ya uenezazi Injili, lakini hakukata tamaa.

Alikufa huko Bremen (Ujerumani) mwaka 865.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  • Pryce, Mark. Literary Companion to the Festivals: A Poetic Gathering to Accompany Liturgical Celebrations of Commemorations and Festivals. Minneapolis: Fortress Press, 2003.
  • Tschan, Francis J. History of the Archbishops of Hamburg-Bremen. New York: Columbia University Press, 1959.
  • Wood, Ian. The Missionary Life: Saints and the Evangelisation of Europe, 400 – 1050. Great Britain: Longman, 2001.
  • Life of Ansgar

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ansgar Mtakatifu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.