Hongwe

(Elekezwa kutoka Ariidae)
Hongwe
Hongwe mweupe (Galeichthys feliceps)
Hongwe mweupe (Galeichthys feliceps)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Siluriformes (Samaki kama kambale)
Familia: Ariidae
Bleeker, 1862
Ngazi za chini

Jenasi 30:

Hongwe, fumi au yahudhi ni samaki wa baharini na maji baridi katika familia Ariidae wa oda Siluriformes ambao wana sharubu ndefu. Wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki duniani kote. Familia hii ina spishi 143.

Maelezo

hariri

Hongwe wana pezimkia lenye panda ndefu. Kwa kawaida jozi tatu za sharubu zipo. Wana magamba ya ufupa juu ya kichwa chao na karibu na pezimgongo lao. Angalau spishi kadhaa zina miiba yenye sumu katika pezimgongo na mapeziubavu.

Msambazo na makazi

hariri

Hongwe sio wa kawaida kati ya samaki kama kambale kwa kuwa huishi hasa katika bahari; nyingi sana za familia za samaki kama kambale huishi katika maji baridi tu na wana uvumilivu mdogo kwa hali ya maji ya chumvi. Hongwe hupatikana katika bahari yenye kina kidogo za kitropiki karibu na pwani za Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, Afrika, Asia na Australia.

Hata hivyo, spishi nyingi kiasi za hongwe zimo pia katika makazi ya maji baridi au hutokea katika maji baridi tu. Huko Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, karibu na spishi 43 huingia maji ya chumvi kidogo au hupatikana katika maji baridi pekee. Na hata katika Afrika spishi kadhaa zinatokea maji baridi hasa.

Ekolojia

hariri

Liche ya makazi yao ya kibahari hongwe wana matohoaji kadhaa ya kipekee ambayo yanawaweka tofauti na samaki wengine kama kambale. Takriban spishi zote ni samaki wanaoatamia mayai kinywani. Madume hubeba idadi ya makumi machache ya mayai madogo kinywani kwa muda wa miezi miwili hadi wachanga watoke na kuanza kuogelea peke yao.

Hongwe huvuliwa sehemu nyingi za Afrika, hata Afrika ya Mashariki. Kwa kawaida huliwa wakiwa wamechomwa au katika supu ya samaki.

Spishi za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri