Atanasi wa Yerusalemu

Atanasi wa Yerusalemu (alifariki Yerusalemu, Palestina, 452 hivi) alikuwa shemasi wa Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu katika jimbo la huko.

Aliteswa vikali sana na mmonaki Theodosi kwa sababu alilaumu uovu wake, akafa kwa kutetea imani sahihi ya Mtaguso wa Kalsedonia[1][2].

Heshima ya watu kwake kama mtakatifu mfiadini ilienea haraka sana.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Julai[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.