Austindo (kwa Kifaransa: Austinde au Ostent; Bordeaux, 1000 hivi - Auch, 1068 hivi) alikuwa askofu mkuu wa Auch, leo nchini Ufaransa, kuanzia mwaka 1049 hadi kifo chake, akijitahidi kueneza urekebisho wa Papa Gregori VII.

Sanamu yake.

Alijenga kanisa kuu pamoja na taifa la Mungu kwa kustawisha maadili [1].

Kabla ya hapo alikuwa mmonaki, halafu abati wa monasteri wa Wabenedikto wa Auch.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Julai[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Alphonse Breuils, Saint Austinde, archevêque d'Auch (1000-1068) et la Gascogne au xie siècle, Auch, impr. de L. Cocharaux, 1895, 365 p.
  • P. Sentez, Notice descriptive et historique de l'église de Sainte-Marie d'Auch ancienne cathédrale, 1818
  • François Bagnéris, La Cathédrale d'Auch et son quartier des chanoines, 1986
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.