Ayo (kwa jina la kuzaliwa Joy Olasunmibo Ogunmakin; amezaliwa katika kitongoji cha mji wa Cologne, Ujerumani, 14 Septemba 1980) ni mwimbaji nchini Ujerumani. Ana asili mchanganyiko: yeye ni binti wa baba Mnigeria na mama anayetokea Romania.

Ayo mwaka 2008.

Maisha

hariri

Anatumbuiza kwa kutumia jina la kisanii la Ayọ au Ayo. Maana yake ni "furaha" kwa Kiyoruba. Bila nukta chini au baada ya "o" neno lamaanisha "kitungu" katika lugha hiyo.

Aliwahi kuishi Ujerumani, Nigeria, Ufaransa, Uingereza na Marekani. Anaishi pamoja na mwimbaji Mjerumani wa muziki ya Reggae Patrice Bart-Williams ("Babatunde") na mtoto wao Nile (*2005)

Albamu

hariri

Albamu yake ya kwanza, 'Joyful', imetolewa mwaka wa 2006. Katika Poland na hata Ufaransa imekuwa ikiuzwa nakala lukuki.

Vibao vyake vilivyo maarufu ni pamoja na 'Down on my knees' ('Nikikupigia Magoti', 2006) na 'And It's Supposed To Be Love' ('Na Hayo Yaelekea Kuwa Mapenzi', 2007).

Albamu 'Gravity At Last' (2008)

Albamu 'Billie-Eve' (2011)

Albamu 'Ticket to The World' (2013)

Albamu 'Ayọ' (2017)

Albamu 'Royal' (2020)

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ayo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.