Bakteriofagi
Bakteriofagi (pia fagi au vilabakteria) ni virusi zinazoambukiza na kujinakili ndani ya bakteria na arkea. Jina hilo linatokana na "bakteria" na neno la Kiyanuni φαγεῖν (fagein), yaani "kula". Bakteriofagi zimeundwa kwa protini ambazo zina jenomu ya ADN au ARN ndani yao, na zinaweza kuwa na miundo ama sahili ama changamano. Jenomu zao zinaweza kusimba jeni chache kama nne (k.m. MS2) au jeni nyingi kama mamia. Fagi hujinakili ndani ya bakteria kufuatia uingizaji wa jenomu zao kwenye sitoplazimu ya bakteria[1].
Bakteriofagi ni kati ya viumbe vya kawaida na anuwai sana katika tabakaviumbe. Bakteriofagi ni virusi za kila mahali zinazopatikana mahali popote bakteria walipo. Inakadiriwa kuna zaidi ya bakteriofagi 1031 kwenye sayari yetu, zaidi kuliko viumbe vingine vyote duniani kwa pamoja, hata pamoja na bakteria. Virusi ni viumbe vya kibiolojia vilivyo vingi kabisa katika safuwima ya maji ya bahari za dunia na sehemu kubwa ya pili ya biomasi baada ya prokarioti, ambapo hadi virioni 9*108 kwa ml zimepatikana kwenye mikeka ya vijiumbe kwenye uso wa maji, na hadi 70% ya bakteria wa baharini wanaweza kuambukizwa na fagi.
Fagi zimetumika tangu mwishoni mwa karne ya 20 kama njia mbadala ya viuavijasumu katika Umoja wa Kisovyeti wa zamani na Ulaya ya Kati na pia katika Ufaransa. Zinaonekana kama tiba inayowezekana dhidi ya aina nyingi za bakteria wenye kukinza dawa kadhaa (angalia tiba kwa fagi). Kwa upande mwingine, fagi za Inoviridae zimeonyeshwa kuimarisha bioutando zinazohusika na nimonia na uvimbe wa fibrosisi na kusitiri bakteria kutoka kwa dawa zilizokusudiwa kutokomeza magonjwa na hivyo kusababisha maambukizo yanayodumu.
Bakteriofagi na usugu wa bakteria kwa dawa
haririUsugu wa bakteria kutosikia dawa za kikemikali umekuwa wa kawaida na kusikika mara kwa mara siku hizi, mambo mengi husababisha usugu huu ikiwemo matumizi mabaya ya dawa[2]. Baadhi ya bakteriofagi pia wamehusishwa na kubeba viini seli vya usugu kutoka kwa bakteria mmoja hadi mwingine. Usugu huu unahusihwa na jinsi bakteriofagi wanapomuingia bakteria na kumuingizia viini vinavyohusika na usugu[3].
Kwa namna nyingine bakteriophagi wanatumika kutibu magonjwa [4] ambayo yanasababishwa na bakteria sugu ambao hawasikii dawa za kikemikali.
Tanbihi
hariri- ↑ "Lytic phage | virus". Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-06-06.
- ↑ "Antibiotic resistance in bacteria well explained" (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-06. Iliwekwa mnamo 2021-06-06.
- ↑ "How do bacteriophages transfer antibiotic resistance genes (ARGs)?".
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-06. Iliwekwa mnamo 2021-06-06.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bakteriofagi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |