Basilika la Mt. Paulo
Basilika la Kipapa la Mt. Paulo Nje ya Kuta ni mojawapo kati ya mabasilika ya zamani na muhimu zaidi ya Roma[1] pamoja na yale ya Mt. Yohane huko Laterano, Mt. Petro huko Vatikano na Mt. Maria huko Eskwilino.
Basilika liko katika eneo la Italia[2], lakini Ukulu Mtakatifu unalimiliki kabisa[3]kama ilivyo kwa maeneo ya balozi za nchi ya kigeni.[4]
Basilika lilianzishwa na kaisari Konstantino Mkuu juu ya mahali (cella memoriae) alipozikwa Mtume Paulo baada ya kukatwa kichwa nje ya ngome ya jiji la Roma.[5][6][7][8][9][10]
Baada ya mabadiliko mengi, lilijengwa upya katika karne ya 19 kwa sababu lilikuwa limeteketezwa na moto. Vipimo vyake ni mita 131.66 kwa 65 kwa 29.70, hivyo ni kanisa la pili kwa ukubwa mjini Roma.
Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake inafanyika kila mwaka tarehe 18 Novemba[11].
Tangu mwaka 1980 Basilika hilo liko katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.
Tanbihi
hariri- ↑ Benedict XVI’s theological act of renouncing the title of "Patriarch of the West" had as consequence that Roman Catholic patriarchal basilicas are today officially known as Papal basilicas.
- ↑ Lateran Treaty of 1929, Article 15 (The Treaty of the Lateran by Benedict Williamson (London: Burns, Oates, and Washbourne Limited, 1929), pages 42-66 Archived 23 Mei 2018 at the Wayback Machine.)
- ↑ Lateran Treaty of 1929, Article 13 (Ibidem Archived 23 Mei 2018 at the Wayback Machine.)
- ↑ Lateran Treaty of 1929, Article 15 (Ibidem Archived 23 Mei 2018 at the Wayback Machine.)
- ↑ the earliest account of a visit to the memorials of the apostles is attributed to Gaius, the Presbyter, "who lived when Zephyrinus was bishop of Rome [AD 199–217]", as quoted by Eusebius reporting that "I can point out the tropaia of the Apostles [Peter and Paul]; for if you go to the Vatican or the Ostian Way, you will find the tropaia of those who founded this Church".
- ↑ "St. Paul's Tomb Unearthed in Rome". National Geographic News. 11 Desemba 2006. Iliwekwa mnamo 21 Julai 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "St Paul burial place confirmed". Catholic News Agency. 2006-12-06. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-20. Iliwekwa mnamo 2013-03-04.
- ↑ "Communiqué about the press conference". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 2016-10-07.
- ↑ "Associated Press: ''Have St. Paul's remains been unearthed?''". MSNBC. 2006-12-07. Iliwekwa mnamo 2013-03-04.
- ↑ Fraser, Christian (2006-12-07). "Christian Fraser, St Paul's tomb unearthed in Rome, BBC News, 7 December 2006". BBC News. Iliwekwa mnamo 2013-03-04.
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo
hariri- Weitzmann, Kurt, ed., Age of spirituality: late antique and early Christian art, third to seventh century, no. 439-440, 1979, Metropolitan Museum of Art, New York, ISBN 9780870991790
- Hinze-Bohlen, Brigitte. Kunst & Architektur-ROM. Cologne: Könemann. Kigezo:Year missing
- Rendina, Claudio (2000). Enciclopedia di Roma. Newton & Compton. ku. 867–868.
- Marina Docci, San Paolo fuori le mura: Dalle origini alla basilica delle origini (Roma: Gangemi Editore 2006).
Viungo vya nje
hariri- The Papal Basilica St Paul Outside-the-Walls, official site.
- "St. Paul-without-the-Walls". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- St. Paul's Tomb Unearthed in Rome on National Geographic News, including a photograph of a side of the sarcophagus.
- The tombs of the apostles: Saint Paul Archived 2013-01-08 at Archive.today
- 3D Model of the church Archived 21 Oktoba 2012 at the Wayback Machine.
- Reliquary of St. Anne's forearm venerated in a side chapel