Benedikta Cambiagio Frassinello

Benedikta Cambiagio Frassinello (Langasco, Genova, 2 Oktoba 1791 - Ronco Scrivia, Genova, 21 Machi 1858) alikuwa mwanamke wa Italia kaskazini ambaye, baada ya kuolewa, aliamua pamoja na mume wake kushika maisha ya kitawa na hatimaye alianzisha shirika la Masista Wabenedikto wa Maongozi ya Mungu kwa ajili ya malezi ya wasichana fukara na wasio na familia [1][2].

Mt. Benedikta alivyochorwa.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 10 Mei 1987 na mtakatifu tarehe 19 Mei 2002.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 21 Machi[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Benedetta Cambiagio Frassinello". Vatican News Services. Iliwekwa mnamo 9 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Saint Benedetta Cambiagio Frassinello". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 9 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.