Bernadi wa Parma (Firenze, Italia, 1060 hivi – Parma, Italia, 4 Desemba 1133) alikuwa mmonaki na mkuu wa urekebisho wa Wabenedikto wakaapweke wa Vallombrosa.

Mt. Bernadi alivyochorwa na Pietro Perugino.

Alifanywa kardinali na askofu wa Parma kuanzia mwaka 1106 hadi kifo chake.

Daima alijitahidi kama mmonaki kulenga ukamilifu wa Kikristo, kama kardinali kulenga ustawi wa Kanisa na kama askofu kulenga wokovu wa watu [1].

Tangu wakati huo aliheshimiwa kama mtakatifu. Mwaka 1139 Papa Inosenti II alithibitisha sifa hiyo [2].

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 4 Desemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/80450
  2. Salvador Miranda. "Uberti, O.S.B.Vall., Bernardo degli (ca. 1060-1133)". The Cardinals of the Holy Roman Church. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-09. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Martyrologium Romanum

Vyanzo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: