Bikira Maria wa Lurdi

(Elekezwa kutoka Bikira Maria wa Lourdes)

Bikira Maria wa Lurdi (kwa Kifaransa: Notre Dame de Lourdes au Notre-Dame-de-Lourdes; kwa Kiingereza "Our Lady of Lourdes") ni jina mojawapo la Bikira Maria lililotokana na njozi maarufu zilizojirudia mwaka 1858 alizozisimulia Bernadeta Soubirous, msichana mnyenyekevu wa Lourdes, Ufaransa.

Bikira Maria akitokea Lourdes akiwa na rosari. Maneno yaliyoandikwa ni ya Kifaransa: Je suis l'Immaculée conception (Ndimi Kukingiwa Dhambi Asili), miaka 4 baada ya Papa Pius IX kutangaza dogma ya Maria Kukingiwa dhambi ya asili.[1]

Binti huyo alisema kwamba aliwezeshwa kumuona mara kadhaa katika pango la Massabielle kati ya milima Pirenei kwenye mto Gave karibu na kijiji cha Lourdes.

Njozi hizo zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika, hata ikaanzishwa kumbukumbu yake katika liturujia kila tarehe 11 Februari, ilipotokea njozi ya kwanza[2]. Kutokana na wingi wa miujiza iliyowatokea wagonjwa wanaohiji huko kwa mamilioni, siku hiyo inaadhimishwa na Kanisa kama Siku ya Kimataifa ya Wagonjwa.

Tanbihi hariri

  1. University of Notre Dame: A Cave of Candles: The Story behind the Notre Dame Grotto. Retrieved on 24 September 2006.
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Lurdi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.