Bikira Maria wa Lurdi
Bikira Maria wa Lurdi (kwa Kifaransa: Notre Dame de Lourdes au Notre-Dame-de-Lourdes; kwa Kiingereza "Our Lady of Lourdes") ni jina mojawapo la Bikira Maria lililotokana na njozi maarufu zilizojirudia mwaka 1858 alizozisimulia Bernadeta Soubirous, msichana mnyenyekevu wa Lourdes, Ufaransa.
Binti huyo alisema kwamba aliwezeshwa kumuona mara kadhaa katika pango la Massabielle kati ya milima Pirenei kwenye mto Gave karibu na kijiji cha Lourdes.
Njozi hizo zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika, hata ikaanzishwa kumbukumbu yake katika liturujia kila tarehe 11 Februari, ilipotokea njozi ya kwanza[2]. Kutokana na wingi wa miujiza iliyowatokea wagonjwa wanaohiji huko kwa mamilioni, siku hiyo inaadhimishwa na Kanisa kama Siku ya Kimataifa ya Wagonjwa.
Tanbihi
hariri- ↑ University of Notre Dame: A Cave of Candles: The Story behind the Notre Dame Grotto. Retrieved on 24 September 2006.
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo
hariri- Harris, Ruth (1999). Lourdes: Body and Spirit in the Secular Age. Penguin Books. ISBN 0-71-399186-0.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Lasserre, Henri (1906). Our Lady of Lourdes (tol. la 11th). New York: P. J. Kenedy & Sons.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Laurentin, L. (1988). "Lourdes". Marienlexikon. Regensburg: Eos Verlag.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help)
Viungo vya nje
hariri- The Glories of Lourdes, full text of book by Justin Rousseil and Joseph Murphy (published 1909)
- The Wonders of Lourdes, full text of book by Louis Gaston de Ségur and Anna Theresa Sadlier (published 1874)
- Our Lady of Lourdes, full text of book by Henri Lasserre (published 1906)
- Pilgrimage of His Holiness John Paul II to Lourdes in 2004, at the Holy See website (archived October 2014)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Lurdi kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |