Botvidi (kwa Kiswidi: Botvid; Södermanland, Uswidi, karne ya 10 – Södermanland, 1120) alikuwa mfanyabiashara ambaye, aliposafiri hadi Uingereza kwa biashara yake, aliongokea Ukristo[1].

Sanamu ya Mt. Botvidi.

Baadaye alitumwa na askofu Sifredi, pamoja na Daudi wa Uswidi[2] na Eskil wa Tuna[3], kama mmisionari nchini kwao akaendelea hadi alipouawa na Mfini ambaye alikuwa kwanza mtumwa na ambaye Botvidi alikuwa amemkomboa, amemfundisha dini na kumbatiza[4].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Julai[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.