Kisaga
Kisaga | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kisaga madoa-manne au wa kunde Callosobruchus maculatus
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Makabila 6:
|
Visaga ni mbawakawa wa nusufamilia Bruchinae katika familia Chrysomelidae. Wadudu hao hujilisha kwa mbegu za spishi za Fabaceae (k.m. maharagwe) na za familia nyingine kadhaa. Hupitia takriban maisha yao yote katika mbegu moja. Familia hii inapatikana duniani kote na ina spishi zaidi ya 4000. Tabia zao zinafanana na zile za vidungadunga (Curculionidae) na kwa hivyo moja ya majina yao kwa Kiingereza ni bean weevils.
Kwa ujumla visaga ni wagumu wenye umbo la duaradufu na vichwa vyao vidogo vimeinamishwa chini. Urefu wao unaanzia mm 1 kufikia mm 22 kwa spishi fulani za kitropiki. Rangi kawaida ni nyeusi na/au kahawia na mara nyingi wana ruwaza ya madoa. Ingawa mandibuli zao zinaweza kurefuka, hawana pua ndefu iliyo sifa ya vidungadunga wa kweli. Mabawa ya mbele ni fupi na hayafikii kabisa ncha ya fumbatio.
Wapevu hutaga mayai juu ya mbegu, kisha mabuu hutafuna tundu la kuingilia mbegu. Wanapokuwa tayari kuwa mabundo, kwa kawaida mabuu hukatia mpevu shimo la kutoka, kisha kurudi kwenye chumba chao cha kujilisha. Visaga wapevu huwa na tabia ya kujifanya kama wamekufa na kuanguka kutoka kwa mmea wakisumbuliwa.
Vidusiwa huwa mimea ya jamii ya kunde (Fabaceae), lakini kuna spishi pia zinazopatikana katika Convolvulaceae, Arecaceae na Malvaceae, na spishi kadhaa huchukuliwa kuwa wasumbufu, k.m. kisaga wa kunde na kisaga wa karanga.
Spishi nyingi ni asili ya Afrika ya Mashariki, k.m. zile zinazoshambulia mbegu za migunga, lakini nyingine zimewasilishwa, kama kisaga wa azuki na kisaga wa njegere.
- Acanthoscelides obtectus, Kisaga wa maharagwe wa Amerika
- Algarobius prosopis, Kisaga wa mrashia
- Bruchus pisorum, Kisaga wa njegere
- Bruchus rufimanus, Kisaga wa maharagwe mapana
- Callosobruchus chinensis, Kisaga wa azuki
- Callosobruchus maculatus, Kisaga wa kunde au kisaga madoa-manne
- Callosobruchus phaseoli, Kisaga wa maharagwe
- Caryedon serratus, Kisaga wa karanga
- Spermophagus albomaculatus, Kisaga madoa-meupe
- Spermophagus incertus
- Spermophagus marmoreus, Kisaga madoadoa
- Zabrotes subfasciatus, Kisaga wa maharagwe wa Meksiko
Picha
hariri-
Kisaga wa maharagwe wa Amerika
-
Kisaga wa njegere
-
Kisaga wa maharagwe mapana
-
Kisaga wa azuki
-
Kisaga wa maharagwe
-
Kisaga wa maharagwe wa Meksiko