Chandra Shekhar Azad

Chandra Shekhar Azad (linatamkwa pia Chandrasekhar; anajulikana kwa wengi kwa jina la Azad, yaani "Uhuru"; 23 Julai 190627 Februari 1931), ni mwanamapinduzi wa India aliyekipanga tena chama cha The Hindustan Republican Association chini ya jina jipya la Hindustan Socialist Republican Association (HSRA) baada ya kifo cha mwanzilishi wake, Ram Prasad Bismil, na viongozi wengine watatu, Roshan Singh, Rajendra Nath Lahiri na Ashfaqulla Khan.

Chandra Shekhar Azad

Mara nyingi alikuwa akitia saini nyaraka za jeshi la HSRA kwa jina la "Balraj" .[1]

Maisha ya awali

hariri

Azad alizaliwa kama Chandrashekhar mnamo 23 Julai 1906 katika kijiji cha Bhabhra. Babu zake walitokea katika kijiji cha Badarka karibu na Kanpur, na mama yake Jagrani Devi Tiwari, alikuwa mke wa tatu wa Sitaram Tiwari, ila wake zake wa kwanza walikufa katika umri wa ujana. Baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza, Sukhdev, huko Badarka, familia ya Sitaram iliamua kuhamia Alirajpur.[2][3]

Mama yake alitaka mtoto wake awe msomi mkubwa wa Sanskrit akamshawishi baba yake ampeleke kwa Kashi Vidyapeeth, Banaras, kusoma, mnamo Disemba 1921, wakati huo Mohandas Karamchand Gandhi alikuwa akizindua Non-Cooperation Movement, Chandra Shekhar, alijiunga. Akiwa na umri wa miaka 15 alikamatwa na kupelekwa mahakamani na baada yA hapo ndipo alikuja kufahamika kwa jina jipya la Azad lenye kumaanisha uhuru katika lugha ya Kihindi.[4]

Maisha ya Kimapinduzi

hariri

Baada ya kusimamishwa kwa harakati za non-cooperation movement (harakati za kutoshirikiana na Waingereza), mwaka 1922, Azad alikutana na mwanamapinduzi kijana, Manmath Nath Gupta, ambaye ndiye aliyemtambulisha kwa Ram Prasad Bismil ambaye alikuja kuanzisha The Hindustan Republican Association (HRA), na kuwa mwanachama hai ambaye alishiriki kwa asilimia kubwa kukusanya pesa za HRA ambazo walizipata kwa njia ya wizi wakiibia serikali. Anahusishwa pia na wizi katika treni ya Kakori mwaka 1925. Watu wengine kama Motilal Nehru mara kadhaa walikuwa wakitoa pesa ili kumuunga Azad mkono katika harakati zao.[5]

Marejeo

hariri
  1. {{cite news|title=MMahatma Gandhi tried his best to save Bhagat Singh |url=https://www.thequint.com/voices/opinion/mahatma-gandhi-tried-his-best-to-save-bhagat-singhs-life |accessdate=4 September 2018 |publisher=The Quint} }
  2. The Calcutta review. University of Calcutta. Dept. of English. 1958. uk. 44. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Catherine B. Asher, mhr. (Juni 1994). India 2001: reference encyclopedia. South Asia Publications. uk. 131. ISBN 978-0-945921-42-4. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Rana, Bhawan Singh (2005). Chandra Shekhar Azad (An Immortal Revolutionary of India). Diamond Pocket Books. ku. 22–24. ISBN 9788128808166.
  5. Mittal, S. K.; Habib, Irfan (Juni 1982). "The Congress and the Revolutionaries in the 1920s". Social Scientist. 10 (6): 20–37. JSTOR 3517065.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chandra Shekhar Azad kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.