Klorini
Klorini ni elementi yenye namba atomia 17 katika mfumo radidia maana yake kiini atomia chake kina protoni 17. Uzani atomia ni 35.453 na alama yake Cl. Ni elementi ya pili katika safu ya halojeni.
Klorini | |
---|---|
Jina la Elementi | Klorini |
Alama | Cl |
Namba atomia | 17 |
Mfululizo safu | Halojeni |
Uzani atomia | 35.453 |
Valensi | 1, 3, 5, 7 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 171.6 K (−101.5 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 239.11 K (−34.04 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.19 % |
Hali maada | gesi |
Katika hali sanifu ni gesi yenye rangi njanokijani. Inamenyuka haraka na elementi nyingine na ni sumu kwa wanyama na binadamu.
Inapatikana kwa wingi katika maji ya bahari kama sehemu ya chumvi ya kawaida NaCl na pia ndani ya chumvi ya KCl.
Matumizi yake ni kusafisha maji au kung'arisha karatasi kiwandani. Imewahi kutumiwa kama sehemu ya silaha kama gesi ya sumu.
Klorini inapotumika kusafisha maji, kuna uwezekano kwamba kiasi cha klorini hubaki mwenye maji. Hivyo basi kuna mbinu mwafaka ambazo hutumika ili kusafisha hayo maji na kuondoa harufu na pia elementi za klorini. Mfano wa baadhi ya hizi mbinu ni uvukizi, klorini dioxide, kubadili myonzo, na njia ya kuchuja.
Picha
hariri-
Klorini katika chupa
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Klorini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |