Panya-maji

Wagugunaji katika familia Muridae
(Elekezwa kutoka Colomys)
Panya-maji
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Colomys
Thomas & Wroughton, 1907
Ngazi za chini

Spishi 4:

Panya-maji ni wanyama wagugunaji wa jenasi Colomys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea Afrika Kusini kwa Sahara katika misitu na savana karibu na vijito, mabwawa na vinamasi.

Maelezo

hariri

Panya hao ni wadogo kiasi. Urefu wa mwili ni sm 11-14 na wa mkia sm 13-19. Uzito ni g 50-75. Manyoya ni kahawia, kuelekea nyuma rangi inakuwa imeiva zaidi. Rangi ya chini ni nyeupe. Manyoya ni mazito na kama mahameli. Mkia mrefu una vigamba lakini manyoya machache tu. Miguu ni mirefu ili kutembea kwenye maji bila kuzama kabisa. Pua imefura kidogo.

Ekolojia

hariri

Panya-maji hukiakia usiku na kulala katika vishimo walivyochimba katika kingo za vijito na mabwawa. Wanatafuta chakula katika maji kame wakitembea ndani yake na kuweka sharubu zao kwenye uso wa maji ili kusikia mitetemo ya mawindo. Hula minyoo, wadudu wa maji, konokono na gegereka wadogo, na pengine vipande vya mimea. Wanaweza kuogelea, lakini wanaifanya tu wakikimbia au kuhama.

Spishi

hariri