Copernici
Copernici (kwa Kilatini: Copernicum, zamani Ununubium) ni elementi sintetiki yenye namba atomia 112 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 277. Alama yake mpya ni Cn (zamani Uub). Si rahisi kutaja tabia zake kwa sababu imetengenezwa mara nne tu katika maabara kama atomi moja-moja.
Copernici (Copernicum, zamani Ununbium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Copernici (Copernicum, zamani Ununbium) |
Alama | Cn (zamani Uub) |
Namba atomia | 112 |
Mfululizo safu | matali za mpito (?) |
Uzani atomia | 277 g/cm³ (kadirio) |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 32, 18, 2 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Asilimia za ganda la dunia | 0% (elementi sintetiki) |
Hali maada | huaminiwa kuwa gesi au kama metali |
Mengineyo | Copernici / Ununubi ni elementi sintetiki yenye nusumaisha mafupi sana iliyotengenezwa mara nne tu |
Jina
haririJina lilitolewa kwa heshima ya mwanaastronomia Nikolaus Kopenikus (kwa Kilatini Copernicus). Jina la awali lilitokana na maneno ya Kilatini kwa "1" (unum) na kwa "2" (bi). Un-un-bi yamaanisha hivyo moja-moja-mbili yaani namba atomia ya elementi. Ununbi lilikuwa jina la muda kabla ya wataaalamu hukubaliana.
Ufumbuzi
haririElementi hiyo iliwahi kutabiriwa na wanasayansi kuwa inaweza kupatikana. Ilitengenezwa mara ya kwanza mwaka 1996 na wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Darmstadt (Ujerumani) kwa kufyatulia viini vya atomi za zinki katika risasi.
Matumizi
haririKama elementi zote za sintetiki, hiyo pia haina matumizi bado: zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena. Kuna uwezekano wa kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu, kutokana na maisha mafupi ya atomi zake, zimeshapotea muda mrefu.
Viungo vya Nje
hariri- WebElements.com - Ununbium
- Apsidium - Ununbium Archived 4 Aprili 2007 at the Wayback Machine.
- Indication for a gaseous element 112 Archived 29 Machi 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Copernici kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |