Shaba

(Elekezwa kutoka Cupri)


Shaba au shaba nyekundu (pia: Kupri au Cupri kama jina la kisayansi) ni elementi yenye namba atomia 29 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 65.54. Alama yake ni Cu.

Shaba au Kupri (cuprum)
Jina la Elementi Shaba au Kupri (cuprum)
Alama Cu
Namba atomia 29
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 65.54
Valensi 2, 8, 18, 1
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1357.77 K (1084.62°C)
Kiwango cha kuchemka 2835 K (2562 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0.01 %
Hali maada mango

Katika mazingira ya kawaida ni metali yenye rangi ya kahawia nyekundu. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1,083 .

Ni kati ya metali za kwanza wanadamu walizotumia baada ya kutoka katika zama za mawe. Si metali ngumu sana, hivyo ilikuwa nyepesi kushughulikiwa na wanadamu wa kale.

Ikichanganywa na stani kunatokea aloi ya bronzi ambayo ni ngumu zaidi. Aloi nyingine ni shaba nyeupe, mchanganyo wa shaba nyekundu na zinki.

Wakati mwingine shaba hupatikana kama metali tupu lakini mara nyingi zaidi kama mtapo.

Tabia muhimu ya shaba ni uwezo wake wa kupitisha umeme. Hivyo imekuwa msingi wa teknolojia yote ya umeme hasa nyaya za kila aina.

Siku hizi shaba huchimbwa hasa katika nchi za Chile (Chuquicamata), Marekani, Urusi, Afrika ya Kati ("Copperbelt" - kanda la shaba), Congo-Zaire, Zambia, Kanada na Peru.