Cuthbert Mayne (Youlston, 1544Launceston, 30 Novemba 1577) alikuwa mchungaji wa Kanisa la Anglikana nchini Uingereza kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki na kupewa daraja takatifu ya upadri.

Padri Cuthberth Mayne.

Alifanya utume wake huko Cornwall hadi alipotangaza hati ya Papa.

Hii ilimsababisha kuuawa chini ya sheria ya malkia Elizabeth I, akiwa mfiadini wa kwanza kati ya wanafunzi wa Seminari ya Kiingereza ya Douai[1].

Mwaka 1970 alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.