Daladala
Daladala ni neno la kawaida nchini Tanzania la kutaja gari dogo linalotumika kwa usafiri wa umma likifuata njia maalumu yenye namba yake.
Dereva anafanya kazi yake pamoja na msaidizi anayeitwa "konda" au "manamba"[1] mwenye kazi ya kukusanya pesa na kufungua au kufunga mlango.
Nchini Kenya magari hayo yanaitwa matatu.
Kwa muda mrefu sasa daladala zimekuwa ni mkombozi wa watu wengi katika kurahisisha shughuli nzima ya usafirishaji. Mwanzoni mabasi yaliyotumika zaidi yalikuwa ni Hiace ambapo Watanzania wakatohoa na kuyaita mabasi hayo "Vihaisi" au "Vipanya".[2] Muda ulivyozidi kwenda hali ikabadilika kwani miji ilikua na kutanuka na watu kuongezeka, hivyo usafiri huo ukawa wa kwenda barabara za ndani huku barabara kubwa zikitawaliwa na mabasi makubwa, haswa mabasi aina ya Costa na Toyota DCM au Dyna Clipper.[3]
Tanbihi
hariri- ↑ Neno "manamba" lina maana nyingi!
- ↑ "Everything you need to know about DalaDalas in Dar es Salaam – the ultimate public transport guide |" (kwa American English). 2023-01-05. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
- ↑ "LATRA | NJia Mpya za Usajili Leseni za Daladala Mkoani Dar es Salaam". www.latra.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-02-05.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Daladala kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |