Damiano wa Pavia (alifariki Pavia, Lombardia, Italia 710 hivi BK) anakumbukwa kama askofu wa 18 wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 680 hivi hadi kifo chake.

Mwaka 679, akiwa bado padri wa Jimbo Kuu la Milano aliandika kwa niaba ya askofu Mansueti wa Milano barua kwa kaisari Konstantino IV kupinga uzushi kuhusu utashi wa Yesu Kristo. Barua hiyo ilisomwa katika Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli.

Alijitahidi kuwavuta watawala Walombardi katika Kanisa Katoliki akawapatanisha na Wabizanti, pia alimaliza farakano la jimbo kuu la Aquileia[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Aprili[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91281
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.