Dini nchini Kenya
Dini nchini Kenya kwa jumla zinaishi kwa amani, ingawa miaka ya hivi karibuni baadhi ya Wakristo waliuawa na wafuasi wa Al Shabaab.
Upande wa takwimu, kulingana na sensa ya mwaka 2009, asilimia 82.5 ya wakazi wa Kenya walikuwa Wakristo (asilimia 47.4 Waprotestanti, asilimia 23.3 Wakatoliki, asilimia 11.8 Wakristo wa madhehebu mengine mbalimbali), asilimia 11.1 ni Waislamu, asilimia 1.6 ni wafuasi wa dini za jadi, asilimia 1.7 ni wa makundi mengine ya dini, na asilimia 2.4 wanadai hawana uhusiano na dini yoyote ile.[1]
Ukristo
haririUislamu
haririAsilimia 60 ya idadi ya Waislamu huishi katika uliokuwa Mkoa wa Pwani, wakiwa asilimia 50 ya jumla ya wakazi wake.
Kaskazini mashariki mwa Kenya kuna takribani asilimia tisini na nane ya Waislamu hasa Wasomali na Waborana.
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "The World Fact Book: Kenya". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-31. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2014.
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu: