Dini asilia za Kiafrika

Dini asilia za Kiafrika ni kati ya dini za jadi ambazo zinadumu hata leo, ingawa wafuasi wake wanapungua mwaka hadi mwaka kulingana na dini zilizotokea Mashariki ya Kati, hasa Ukristo na Uislamu, ambazo zinazidi kuenea barani Afrika.

Dini za Kiafrika zinafuata imani maalumu, sawa kabisa na hizo za nchi za ughaibuni ambazo zimeleta mfumo mpya wa kuabudu. Badala ya kuabudia mapangoni au misituni kama Waafrika walio wengi walivyofanya kwa karne nyingi, zimehimiza kujenga makanisa na misikiti kwa ajili ya kumwabudu Mungu kadiri ya ufunuo wake mwenyewe.

Madhehebu mengi ya Kikristo yamekuwa yakimuabudu Mungu kwa kushirikiana na wafu wanaoheshimiwa kama watakatifu, wakati Waafrika tangu zamani waliwaenzi wazee wao waliokufa na kuwaita mizimu. Waafrika hao tangu zamani waliwaheshimu wafu kwenye makaburi yao, lakini baadhi ya Wakristo waliwaheshimu wafu kanisani kwa sala zao pamoja na kusujudu pengine masalia au picha za hao wafu.

Katika Amri Kumi za Biblia, Waafrika kwa jumla walikuwa nazo hata kabla ya kuja kwa Wazungu: walijua kwamba imewapasa kuwaheshimu wazazi wao, kutoua, kutoiba wala kufanya kinyume na maagizo ya wazee wao.

Kwa mtazamo wa Kikristo, Mungu mwenyewe ndiye aliyewaandaa hivyo Waafrika kupokea wokovu kwa njia ya Yesu Kristo, aliyekuja si kutangua bali kukamilisha yale yote yaliyo mema katika binadamu wote.

Pamoja na hayo yote, bado baadhi ya makabila yanaendelea na mila zao za kuheshimu wafu ingawa dini zenye asili ya Mashariki ya Kati zinakataza namna hiyo.

Icon-religion.svg Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.