Droktovei (530 hivi - 580 hivi) alikuwa mmonaki nchini Ufaransa anayetajwa kama mfuasi wa Jermano wa Paris ambaye, baada ya kuchaguliwa kuwa askofu, alimchukua naye, halafu akamweka kuongoza monasteri mpya mjini Paris ambayo chini yake ilistawi sana[1].

Venansi Fortunati alimsifu sana katika kitabu chake "Carmina"[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Machi[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.