Edin Dzeko

(Elekezwa kutoka Edin Džeko)

Edin Džeko (amezaliwa 17 Machi 1986) ni mchezaji wa kandanda mwenye uraia wa Kibosnia na ambaye ni mshambuliaji katika klabu ya A.S. Roma na timu ya taifa ya Bosnia na Herzegovina.

Edin Džeko
Youth career
1996–2003Željezničar
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2003–2005Željezničar20(1)
2005–2007Teplice43(16)
2005Ústí nad Labem (loan)15(6)
2007–Wolfsburg77(41)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2005–2007Bosnia and Herzegovina U-212(1)
2007–Bosnia and Herzegovina23(14)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 19 Desemba 2009.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 15 Novemba 2009

Wasifu wa Klabu

hariri

Wasifu wa Mapema

hariri

Džeko alicheza mechi yake ya kwanza ya utaaluma(professional) katika klabu ya FK Željezničar, na alicheza kama mchezaji wa kiungo cha kati kuanzia mwaka ya 2003 hadi 2005 lakini alifunga bao moja tu kutoka jumla ya mechi 40 alizocheza. Alikopwa katika klabu ya Ústí nad Labem mwaka wa 2005, na alifunga mabao sita kutokana na mechi 15 alizocheza akiwa katika klabu hiyo. Baadaye mwaka huo, alihamia klabu ya Czech ya FK Teplice, na aliichezea klabu hiyo hadi mwaka wa 2007 na alifunga mabao 16 katika mechi 28 alizozicheza. Alikuwa mchezaji mwenye idadi nyingi ya mabao katika ligi hiyo ya kandanda ya Czech katika msimu wa 2006-07. Kutokana na mchezo wake bora na wa hali ya juu, meneja wa zamani wa timu ya VfL Wolfsburg, Felix Magath, alimsaini kwa kitita cha yuro (€ ) milioni 4.

Wolfsburg

hariri

Baada ya kuhamishwa kwenda Wolfsburg, Džeko alionyesha makali yake pamoja na ujuzi wake punde tu alipowasili kwa kufunga mabao tano na kuandaa pasi tatu zilizosababisha mabao katika michezo 11 alizozicheza. Pia aliteuliwa na Sportal kama mshambuliaji bora katika nusu ya kwanza ya msimu wa 2007-08 katika ligi hiyo ya Bundesliga. Katika msimu wake wa kwanza nchini Ujerumani, Katika msimu wake wa kwanza nchini Ujerumani, Wolfsburg walimaliza katika nafasi ya tano, na kufuzu kushiriki katika Kombe la UEFA la msimu wa 2008-09. Džeko alimaliza msimu wa 2007-08 akiwa na mabao nane na pasi saba zilizosababisha mabao katka mechi 17 alizoanza.

Wolfsburg walipomnunua mchezaji mwenzake mwenye uraia wa Kibosnia, Zvjezdan Misimović, mchezo wa Džeko ulilipuka na kuwa hwa hali ya juu zaidi katika msimu wa pili. Licha ya mchezo usiyoridhisha katika nusu ya kwanza ya msimu, yeye na timu yake walipata fomu zao na walishinda ligi yao ya kwanza ya Bundesliga. Mnamo Mei 2009, Džeko alifunga mabao tatu dhidi ya Hoffenheim, na mabao mengine tatu dhidi ya Hannover 96 wiki mbili tu baadaye, na kuchangia kuelekea kumaliza kwa nguvu kwa msimu wa 2008-09. Alimaliza msimu huo kwa jumla ya mabao 26 ya ligi, na jumla hii ilikuwa ya pili, ya kwanza ikiwa ya mchezaji mwenzake, Grafite. Pamoja na Grafite, walifomu ushambulizi wa wachezaji wawili uliofanikiwa sana katika historia ya Bundesliga. Alimaliza msimu wa 2008-09 na mabao 26 na pasi 10 zilizosababisha mabao katika mechi 32 alizocheza. Katika DFB-Pokal, alikuwa na mabao sita katika mechi mbili tu, na katika Kombe la UEFA, alikuwa na mabao nne na pasi 4 zilizosababisha mabao katika mechi nane. Mchezo wake ulimsaidia kutuzwa tuzo la "Mchezaji kandanda wa mwaka wa wachezaji" wa Bundesliga. Licha ya kuvutia riba kutoka kwa klabu ya AC Milan, maafisa wa Wolfsburg walimshawishi Džeko kukaa kwa kuifanya upya mkataba wake hadi Juni 2013.

Alifunga bao lake la kwanza la kombe la mabingwa barani Ulaya la UEFA mnamo 30 Septemba 2009 dhidi ya Manchester United katika mechi waliopoteza 2-1 katika uwanja wa Old Trafford. Alikuwa mmoja wa wachezaji 30 walioteuliwa kwa tuzo la Ballon d'Or (mchazaji kandanda bora barani Ulaya) la mwaka wa 2009.

Wasifu wa Kimataifa

hariri

Džeko aliichezea nchi yake kwa mara ya kwanza akiwa katika timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 19 ya Bosnia na Hercegovina. Pia alijumuishwa katika kikosi cha vijana wasiozidi umri wa miaka 21 na alicheza mechi ya mchujo ambayo Uholanzi ilikuwa mwenyeji wake mwaka wa 2007. Changamoto za kwanza za Bosnia katika shindano hili zilikuwa Armenia na Norway. Waliicharaza Armenia kwa mabao 3-2 na walitoka sare ya 1-1 na Norway, hivyo basi walifuzu kushiriki katika mechi ya mchujo dhidi ya Jamhuri ya Czech. Katika mechi ya wa kwanza, Bosnia ilipoteza 2-1; mechi ya pili ilikamilika kwa sare ya 1-1. Džeko alifunga mabao mengi katika shindano hili.

Aliichezea timu kuu ya taifa kwa mara ya kwanza dhidi ya Uturuki tarehe 2 Juni 2008. Hii ilikuwa mechi ambayo mchezaji huyu atakumbuka, kwani alifunga bao muruwa kutoka nje ya eneo la penalti wakati wa muda ya ziada wa nusu ya kwanza ya mechi. Bao hilo lilisawazisha tokeo kuwa 2-2, kisha Bosnia wakaishinda mechi hiyo 3-2. Alifunga mabao tisa katika mechi za kufuzu kushiriki katika Kombe la Dunia la FIFA 2010 na kumaliza kama mfungaji wa pili bora katika mechi za kufuzu za UEFA, pamoja na Wayne Rooney wa Uingereza, wote hawa wawili wakiwa nyuma ya mshambuliaji wa Ugiriki, Theofanis Gekas, aliyekuwa na mabao 10.

Takwimu ya Wasifu

hariri
As of 11 Desemba 2009
Club performance Ligi Kombe Continental Total
SeasonClubLeague AppsGoalsAppsGoals AppsGoals AppsGoals
Bosnia-Herzegovina LeagueKup Bosne i Hercegovine Ulaya Total
2004–05 Željezničar Premier League 20 1 0 0 0 0 20 1
Czech Republic LeagueCzech Republic Football Cup Ulaya Total
2005–06 Ústí nad Labem Czech 2. Liga 15 6 0 0 0 0 15 6
2005–06 Teplice Gambrinus liga 13 3 0 0 0 0 13 3
2006–07 30 13 0 0 0 0 30 13
Germany LeagueDFB-Pokal Ulaya Total
2007–08 Wolfsburg Fußball-Bundesliga 28 8 5 1 0 0 33 9
2008–09 32 26 2 6 8 4 42 36
2009–10 17 7 2 2 6 4 25 13
Total Bosnia-Herzegovina 20 1 0 0 0 0 20 1
Czech Republic 58 22 0 0 0 0 58 22
Germany 75 40 9 9 14 8 98 57
Career Total 136 63 9 9 14 8 178 80

Mabao ya kimataifa

hariri
# Tarehe Mahali Mpinzani Mabao Matokeo Mashindano
1. 2 Juni 2007 Uwanja wa Kosevo, Sarajevo Uturuki 2 -2 3-2 Mechi ya kufuzu kushiriki katika EURO
2. 10 Septemba 2008 Bilino polje,Zenica Estonia 5 -0 7-0 Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
3. 10 Septemba 2008 Bilino polje,Zenica Estonia 6 -0 7-0 Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
4. 11 Oktoba 2008 Uwanja wa BJK İnönü Stadium,Istanbul Uturuki 0-1 2-1 Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
5. 15 Oktoba 2008 Bilino polje,Zenica Armenia 2 -0 4-1 Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
6. 20 Novemba 2008 Stadion Ljudski vrt,Maribor Slovenia 3-4 Mechi ya kirafiki
7. 28 Machi 2009 Uwanja wa Cristal Stadium, Genk Ubelgiji 0-1 2.4% Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
8. 17 Aprili 2009 Bilino polje,Zenica Ubelgiji 1 -0 2-1 Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
9. 17 Aprili 2009 Bilino polje,Zenica Ubelgiji 2 -0 2-1 Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
10. 6 Juni 2009 Stade Pierre de Coubertin, Cannes Oman 1 -0 2-1 Mechi ya kirafiki
11. 12 Agosti 2009 Uwanja wa Kosevo, Sarayevo Irani 1 -0 2.3 Mechi ya kirafiki
12. 12 Agosti 2009 Uwanja wa Kosevo Sarajevo Irani 2 -0 2.3 Mechi ya kirafiki
13. 10 Oktoba 2009 {A. Le Coq Arena,Tallinn Estonia 0-1 0.2% Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010
14. 14 Oktoba 2009 Bilino polje, Zenica Uhispania 2 -5 2-5 Mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la 2010

Wolfsburg

  • Bundesliga: 2008-09

Kibinafsi

  • "Mchezaji kandanda wa mwaka wa wachezaji" wa Bundesliga wa msimu wa 2008-09
  • Nafasi ya 13 kwa Ballon d'Or wa mwaka 2009

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: