Hanithi

(Elekezwa kutoka Elopidae)
Hanithi
Hanithi wa Atlantiki (Elops saurus)
Hanithi wa Atlantiki (Elops saurus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii
Oda: Elopiformes
Familia: Elopidae
Bonaparte, 1832
Jenasi: Elops
Linnaeus, 1766
Ngazi za chini

Spishi 7 zilizopo:

Hanithi, hanisi au mkizi ni samaki wa baharini wa jenasi Elops katika familia Elopidae. Jina la Kiingereza, “tenpounder”, ni kioja kwa sababu uzito wa kipeo wa samaki hawa ni kg 10.

Hanithi ni samaki wakazi wa pwani yanayopatikana katika maeneo ya tropiki na nusutropiki, na mara kwa mara huingia katika maji ya wastani. Kutaga mayai na kuunganisha na shahawa kunafanyika baharini na lava wa samaki huhamia barani katika maji ya chumvi kidogo. Chakula chao ni samaki wadogo na gegereka (uduvi). Kwa kawaida ukubwa wa kipeo wa spishi zote ni takriban m 1 na uzito wa kipeo kg 10. Mwili una umbo la dulabu na mkato wa upande hadi upande una umbo la yai. Macho yao ni makubwa na yamefunikwa kwa sehemu kwa kope nono.

Kama wale wa mikunga, lava ni wa uwazi, wenye kusisitiza na kama utepe. Baada ya ukuaji wa awali, hupungua na kisha hupangilia katika maumbile ya waliokomaa.

Familia hii inavuliwa lakini mwili una miiba mingi na kwa hiyo samaki hawa hawafai sana kwa ulaji. Huvuliwa na kutumika kama chambo au wanaweza kusagwa kwa makusudi ya unga wa samaki.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Spishi za kabla ya historia

hariri
  • Elops bultyncki
  • Elops miiformis

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hanithi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.