Felician V. M. Nkwera
Felician Venant Nkwera (alizaliwa Luilo, leo katika Wilaya ya Ludewa, mkoa wa Njombe[1], 28 Aprili 1936 ) ni padri aliyetengwa na Kanisa Katoliki [2] na mwandishi nchini Tanzania.
Felician V. M. Nkwera | |
Amezaliwa | 28 Aprili 1936 Lwilo |
---|---|
Nchi | Tanzania |
Makazi | Riverside, Dar es salaam |
Anafahamika kwa | Padri Mwasisi wa Kituo Cha Maombezi cha mAma Bikira Maria |
Maisha yake
haririWazazi wa Padri Nkwera walikuwa ni Venant Nkwera (baba) na Emmaculata Mhagama (mama).
Alipata upadirisho mwaka 1968 akaanza huduma ya maombezi akiwa bado padri kijana mkoani Tabora na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam. Ni huduma ambayo imemfanya awe kwenye mgogoro mkubwa na jimbo alilokuwa akilihudumia wakati huo; mgogoro huo ukafika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na baadaye Roma.
Ni huduma ambazo wenye imani wamekuwa wakikiri kwa kinywa na maandishi kwamba wameponywa huku rozari, maji ya baraka na sala vikiwa ndio msingi mkuu wa maombi yaliyopelekea kuponywa huko. Shuhuda za uponywaji wa wagonjwa zinaandikwa ama kusimuliwa na wahusika wenyewe.[3]
Muda mrefu umepita tangu Padri Nkwera asimamishwe kuhudumia Kanisa. Baadhi wanakosoa huduma hizi za maombezi, hasa wakiangazia namna sakata hili lilivyoanza. Baadhi wanaangalia sababu kuu ni ukaidi, huku wakiainisha bayana kwamba Padri Nkwera hakuwa mtii kwa aliyekuwa kiongozi wake kwa wakati huo alipokuwa akilihudumia Jimbo Katoliki la Njombe na zaidi hakutii maamuzi na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wake wakubwa yaani maaskofu, Baraza la Maaskofu na hata Kardinali Polycarp Pengo kwa wakati huo.[4]
Kesi mahakamani
haririPadri Felician V. Nkwera amekuwa na kesi nyingi mahakamani huku baadhi ya waumini au wafuasi wake pia wakiwa na kesi zenye sura tofautitofauti.
Vitabu na machapisho yake
haririTanbihi
hariri- ↑ kabla ya Kuundwa kwa Mkoa huo, Njombe ilikuwa ni Wilaya ndani ya Mkoa wa Iringa
- ↑ https://peacefulsocieties.uncg.edu/2010/06/24/dissident-catholic-cult-simmers-in-fipa-territory/#:~:text=The%20story%20goes%20back%20to,Madunda%20Parish%2C%20in%20northern%20Tanzania. https://peacefulsocieties.uncg.edu/2010/06/24/dissident-catholic-cult-simmers-in-fipa-territory/#:~:text=The%20story%20goes%20back%20to,Madunda%20Parish%2C%20in%20northern%20Tanzania.
- ↑ https://ixtheo.de/Record/1571447695/Description#tabnav
- ↑ https://kiongozi.tripod.com/maonimc2.html
- ↑ https://search.worldcat.org/title/tumbuizo-la-jioni-kimetungwa-na-felician-vi-nkwera/oclc/479562544
- ↑ https://searchworks.stanford.edu/view/170373
- ↑ https://books.google.co.tz/books/about/Maana_na_lengo_la_adhabu_ya_kifungo.html?id=K6lJAAAACAAJ&redir_esc=y
- ↑ https://bookpremiumfree.com/downloads/nadharia-za-kuhakiki-fasihi/
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |