Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (kwa Kiingereza Tanzania Episcopal Conference, TEC) ni muundo wa Kanisa Katoliki unaokutanisha maaskofu wake wote wa nchi ya Tanzania, wakiwa wanaongoza jimbo, au ni waandamizi, wasaidizi au wamestaafu.
Katiba ya Baraza ilipitishwa na Ukulu mtakatifu tarehe 8 Januari 1980.
Makao makuu yako Dar es Salaam, mtaa wa Kurasini, lakini kuna mpango wa kuyahamishia Dodoma, mji mkuu wa nchi.
TEC ni kiungo cha Association of Member Episcopal Conferences in Eastern Africa (AMECEA) na cha Symposium of Episcopal Conferences of Africa and Madagascar (SECAM).
Orodha ya marais wake
hariri- 1969-1970: Placidus Gervasius Nkalanga, askofu wa Bukoba
- 1970-1976: James Dominic Sangu, askofu wa Mbeya
- 1976-1982: Mario Epifanio Abdallah Mgulunde, askofu wa Iringa
- 1982-1988: Anthony Mayala, askofu wa Musoma
- 1988-1994: Josaphat Louis Lebulu, askofu wa Same
- 1994-2000: Justin Tetmu Samba, askofu wa Musoma
- 2000-2006: Severine Niwemugizi, askofu wa Rulenge-Ngara
- 2006-2012: Juda Thadaeus Ruwa'ichi, askofu mkuu wa Mwanza
- 2012-2018: Tarcisius Ngalalekumtwa, askofu wa Iringa
- 2018- ...: Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, askofu wa Mpanda.
Viungo vya nje
hariri- (Kiingereza) Tovuti ya Baraza Archived 11 Oktoba 2011 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) Kanisa Katoliki Tanzania katika Gcatholic
- (Kiingereza) Kanisa Katoliki Tanzania katika tovuti ya Catholic Hierarchy
- Hati ya Kilatini Quantum grata, AAS 60 (1968), uk. 521