Felisi na Regula
Felisi na Regula (walifariki 286) ni Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao.
Inasemekana walikuwa askari wa jeshi la Roma ya Kale walioongozwa na Morisi Mtakatifu[1].
Kufuatana na mapokeo ya karne ya 4 kikosi hicho kilijumlisha wanajeshi Waafrika kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo. Katika mapokeo ya sanaa ya Kikristo walichorwa kama Waafrika weusi.
Huko Agaunum (leo Saint-Maurice-en-Valais), karibu na mto Rhone, katika eneo la Uswisi wa leo, walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye karibu kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.
Ndugu Felisi na Regula walinusurika kwa kukimbia ila wakaja kuuawa baadaye huko Zurich (Uswisi vilevile), inasemekana pamoja na wenzao 66.
Waliheshimiwa mapema kama watakatifu wafiadini pamoja na mtumishi wao Esuperansi [2].
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 11 Septemba[3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography, Literature, Sects and Doctrines (1880), 439.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/92463
- ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |