Sanaa ya Kikristo
Sanaa ya Kikristo ni sanaa iliyokusudiwa kutokeza imani ya Ukristo katika uzuri wake. Mara nyingi hiyo inafanyika kuhusiana na ibada na majengo yanayotumika kwa ajili hiyo.

Kwa ajili hiyo inatumia mada na mifano ya Injili au vitabu vitakatifu vingine, lakini pia habari za maisha ya watakatifu.
Madhehebu karibu yote yanatumia sanaa za aina fulani kwa namna hiyo, ingawa mengine yanakataa uchoraji n.k.
Picha za Yesu ndiyo michoro ya kawaida zaidi, zikifuatwa na zile za Bikira Maria katika Kanisa Katoliki na yale ya Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki.
Kutokana na kujali na kustawisha aina zote za sanaa, Wakatoliki wameshika nafasi ya kwanza katika idadi ya vituo vilivyoorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia. Kwa mfano, nchi nzima ya Vatikani imo katika orodha hiyo.
Wakatoliki katika Mtaguso II wa Vatikano (hati Sacrosanctum Concilium) walikiri kwamba muziki wa Kikristo ndio sanaa bora kuliko zote kwa sababu unahusiana zaidi na Neno la Mungu ambalo unalipamba kwa noti ili lieleweke na kugusa mioyo zaidi.
TanbihiEdit
MarejeoEdit
- Grabar, André (1968). Christian iconography, a study of its origins. Princeton University Press. ISBN 0-691-01830-8.
- Régamey, Pie-Raymond (1952). Art sacré au XXe siècle? Éditions du Cerf.
- Evans, Helen C. & Wixom, William D. (1997). The glory of Byzantium: art and culture of the Middle Byzantine era, A.D. 843-1261. New York: The Metropolitan Museum of Art. ISBN 9780810965072.
- Hein, David. “Christianity and the Arts.” The Living Church, May 4, 2014, 8–11.
Viungo vya njeEdit
- Princeton's Index of Christian Art Archived Oktoba 30, 2007 at the Wayback Machine.
- Society for the Arts in Religious and Theological Studies
- Christians in the Visual Arts
- Biblical Art on the WWW - a database of Biblical images
- Age of spirituality : late antique and early Christian art, third to seventh century from The Metropolitan Museum of Art
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sanaa ya Kikristo kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |