Fidel Alejandro Castro Rúz (13 Agosti 1926 - 25 Novemba 2016) alikuwa kiongozi wa Kuba tangu mwaka 1959 hadi 2006 akiwa waziri mkuu hadi 1976 halafu rais wa nchi.

Fidel Castro

Maisha

hariri

Fidel Castro alisoma sheria kwenye chuo kikuu cha Havana akawa wakili kabla ya kujiunga na siasa ya mapinduzi. Castro aliongoza harakati ya upinzani wa wanamgambo dhidi ya udikteta wa jenerali Fulgencio Batista tangu 1953.

Fidel Castro alivyokamatwa baada ya uvamizi wa Moncada, mwaka 1956.

Hatimaye mwaka 1958 alishinda jeshi la Batista aliyelazimika kukimbia nchi tarehe 1 Januari 1959. Fidel Castro alitakiwa kuuawa na jeshi la Batista lakini alikimbia na kuvuka bahari ya Atlantiki hadi Mexico umbali wa kilomita 100. Baada ya muda alipanda mashua hadi Arjentina ili kupata msaada wa Che Guevara aliyekuwa tabibu akamsaidia Castro kupambana dhidi ya Batista na mara baada ya kumshinda Fidel Castro alikuwa Rais, Ernesto che Guevala akiwa waziri wake. Hivyo Castro akawa kiongozi mpya wa Cuba hadi mwaka 2006.

Castro hakukubaliwa na Marekani, hivyo akajiunga na siasa ya Umoja wa Kisovyeti dhidi ya Marekani. Aliongoza harakati yake kuwa chama cha kikomunisti akatangaza ukomunisti mwenyewe.

Hata baada ya kuporomoka kwa ukomunisti kote duniani (1989) aliendelea kutawala kwa kufuata mfumo huo. Baada ya upasuaji alioupata tarehe 31 Julai 2006 alikabidhi madaraka kwa mdogo wake Raul Castro.

Alifariki tarehe 25 Novemba 2016.