Open main menu
Mtakatifu Mama Frances Xavier Cabrini

Fransiska Saviera Cabrini (Sant'Angelo Lodigiano, Italia, 15 Julai 1850Chicago, Illinois, Marekani, 22 Desemba 1917) alikuwa mwanzilishi wa shirika la Masista Wamisionari wa Moyo Mtakatifu (kwa Kiingereza Missionary Sisters of the Sacred Heart).

Jumuiya hiyo ilianzia Italia na kufanya kazi hasa Marekani kati ya wahamiaji kwa kujenga shule, hospitali na nyumba kwa watoto yatima.

Mwaka 1946 Mama Cabrini alitangazwa kuwa mtakatifu akiwa raia Mmarekani wa kwanza kupewa heshima hiyo.

Sikukuu yake ni tarehe 22 Desemba.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit