Fuljensi wa Ecija
Fuljensi wa Ecija (alifariki 630) alikuwa askofu huko Andalusia, nchini Hispania, ndugu wa Leandro, Isidoro na Florentina. Kwa ajili yake Isidoro aliandika kitabu juu ya vyeo vya Kikanisa.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Januari[1].