Leandri wa Sevilia

Leandri wa Sevilia (Cartagena, leo nchini Hispania, 534 hivi - Sevilia, Hispania, 13 Machi 600 au 601) alikuwa askofu mkuu wa Sevilia ambaye kwa mahubiri na juhudi zake alifaulu kuingiza katika Kanisa Katoliki kutoka Uario Wavisigoti waliotawala Hispania na Ureno wa leo, kuanzia Hermengildi na Rekaredo, watoto wa mfalme.

Mt. Leandro alivyochorwa na Bartolomé Esteban Perez Murillo.

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Machi[1] au 27 Februari.

Maisha

hariri

Alizaliwa na Severianus na Turtura huko Cartagena, Hispania, mwaka 534 hivi, akiwa wa kwanza kati ya watoto watano, ambao wanne kati yao wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu: Leandri, Fulgensi, Florentina wa Cartagena na Isidori wa Sevilia. Kati yao, watatu walikuwa maaskofu, na wa kike alikuwa mtawa.

Leandro, akiwa msomi aliyeshika maisha magumu kama Mbenedikto, ni maarufu pia kama mwanzilishi wa shule katoliki na mlezi wa mdogo wake Isidori aliyewarithisha hasa watu wa Ulaya Magharibi wa Karne za Kati elimu ya kale. Ndiye aliyemlea kwa nidhamu kubwa baada ya kifo cha baba yao, akimtengenezea mazingira ya kimonaki ambamo awajibike katika masomo akitumia maktaba yao kubwa ili kujiandaa akabili matatizo ya wakati ule.

Baada ya kuwa askofu, juhudi zake za kuleta rasi yote katika Ukatoliki zilifanya apelekwe uhamishoni.

Maandishi

hariri

Mwandishi bora kuliko mdogo wake Isidori, vimetufikia vitabu vyake viwili tu: De institutione virginum et contemptu mundi, kanuni ya kimonaki kwa ajili ya dada yake, na Homilia de triumpho ecclesiæ ob conversionem Gothorum (P.L., LXXII).

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.