Gordio wa Kaisarea
Gordio wa Kaisarea (alifariki 304) ni Mkristo aliyefia dini yake huko Kaisarea wa Kapadokia (leo nchini Uturuki) wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano.
Gordio alikuwa akida aliyeacha jeshi la Roma ili asifanye dhambi, akaishi mlimani na hatimaye akarudi mjini alipouawa kwa sababu alimkiri Yesu kuwa Mwana wa Mungu[1].
Basili Mkuu alitoa hotuba juu yake akiripoti ushahidi wa waliokuwepo.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |