Korobindo (Passeridae)

(Elekezwa kutoka Gymnoris)
Korobindo
Korobindo koo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Passeridae (Ndege walio na mnasaba na shomoro)
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 6:

Korobindo ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Passeridae. Kuna ndege wengine ambao wanaitwa korobindo katika familia Ploceidae. Spishi za ukurasa huu zinatokea Afrika isipokuwa (Chestnut-shouldered Petronia) ambaye anatokea Asia. Korobindo-mawe anatokea Ulaya pia na korobindo-msitu na korobindo hudhurungi Asia pia. Ndege hawa wanafanana na shomoro, lakini rangi yao ni vivu zaidi. Madume wa jenasi Gymnoris wana doa njano chini ya koo ambalo ni ngumu kuona kwa kawaida. Hula mbegu, beri, mbochi na wadudu. Wanalijenga tago lao kwa nyasi na manyoya katika tundu mtini au pengine ukutani. Jike huyataga mayai 3-5.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi ya mabara mengine

hariri