Heribert wa Cologne
Heribert wa Cologne (kwa Kijerumani: Heribert von Köln; Worms, Ujerumani, 970 hivi; Cologne, Ujerumani 16 Machi 1021) alikuwa Chansella wa Dola Takatifu la Roma chini ya kaisari Otto III.
Alipochaguliwa kuwa Askofu mkuu wa Cologne, kinyume cha matakwa yake, aliangaza mfululizo waklero na walei kwa mifano yake ya uadilifu, aliouhamasisha kwa mahubiri yake pia.
Aliheshimiwa sana akiwa hai akatangazwa na Papa Gregori VII kuwa mtakatifu mwaka 1075 hivi.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, 16 Machi[1].
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Heribert von Köln (with picture of shrine) (Kijerumani)
- http://www.catholic.org/encyclopedia/view.php?id=205
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |