Hilarioni Kijana (alifariki 845) alikuwa mmonaki padri mkuu wa monasteri huko Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, aliyedhulumiwa na kaisari wa Bizanti kwa sababu ya kutetea heshima kwa picha takatifu. Kwa ajili hiyo alifungwa, alipigwa mijeledi na kupelekwa uhamishoni, lakini hakubadili msimamo wake [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Juni[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.