Domodomo
Domodomo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Domodomo wa Peters (Gnathonemus petersii)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 21:
|
Domodomo ni samaki wa maji baridi wa nusufamilia Mormyrinae katika familia Mormyridae na ngeli Actinopterygii (mapezi yenye mihimili) ambao wanatokea Afrika tu. Spishi nyingi zina pua ndefu na/au mdomo wa chini mrefu. Kwa hivyo inaonekana kama zina aina ya mwiro na kwa sababu ya hiyo jina lao kwa Kiingereza ni “elephantfish”, “tapirfish” au “trunkfish”. “Mwiro” huo hutumika kwa kusikia invertebrata katika matope. Spishi zenye pua au mwiro mfupi kiasi huitwa mputa kwa kawaida. Majina mengine ni linjolo, mbete, mbelewele, mpuni, nchemba, ndaka na ntachi.
Nusufamilia hii ina zote ila moja za jenasi za Mormyridae. Ni nusufamilia kubwa kabisa katika oda Osteoglossiformes ikiwa na takriban spishi 170. Spishi hizi zina uwiano mkubwa kati ya masi ya ubongo na ile ya mwili kwa sababu ubongonyuma umevimba na hutumika katika udakaji wao wa umeme. Zaidi ya hao zinajulikana kwa kushikilia rekodi ya zoolojia ya takriban 60% iliyo ni asilimia ya nishati unayotumia ubongo wao ikilinganishwa na mwili mzima. Kabla ya ugunduzi huu, ilikuwa ubongo wa kibinadamu ambao ulifikiriwa kushikilia rekodi hii lakini kwa ukweli hutumia 20% tu.
Ukubwa wa ubongo
haririUbongo katika wanyama wazima hutumia nishati katika kiwango cha 2% hadi 8% kama asilimia ya nishati ya mwili mzima bila kujali ukubwa wa mwili. Mbongo za wanyama pekee zinazotumia zaidi ya 10% (kwa kigezo cha ulaji wa oksijeni) ni zile za nyani wachache (11-13%) na wanadamu. Lakini utafiti uliochapishwa mwaka wa 1996 katika Journal of Experimental Biology na Göran Nilsson wa Chuo Kikuu cha Uppsala iligundua kwamba mbongo za domodomo zinatumia takriban 60% ya matumizi yao ya oksijeni ya mwili. Hii ni kwa sababu ya mchanganyiko wa ubongo mkubwa (3.1% ya masi ya mwili ikilinganishwa na 2% kwa mwanadamu) na wao kuwa ektothermiki.
Matumizi ya nishati ya mwili ya wanyama ektothermiki ni takriban 1/13 ya yale ya endothermiki lakini matumizi ya nishati ya mbongo za wanyama ektothermiki na endothermiki ni sawa. Kuna wanyama wengine walio na ubongo wa asilimia kubwa (2.6-3.7% ya masi ya mwili) kama vile popo, mbayuwayu, kunguru na shomoro lakini hawa pia wana umetaboli mkubwa wa nishati ya mwili. Matumizi makubwa ya nishati ya ubongo ya domodomo, yasiyo ya kawaida, yanatokana katika mchanganyiko usio wa kawaida wa ubongo mkubwa katika mwili wa matumizi madogo ya nishati. Oksijeni kwa hili katika mahali pa oksijeni ya chini hutoka kwa kuchochea hewa kwenye uso wa maji.
Udakaji wa umeme
haririKinyume na mamalia sehemu ya ubongo iliyovumba katika domodomo ni ubongonyuma sio ubongombele. Ubongonyuma huu unahusianisha na udakaji wa umeme. Wanazalisha nyuga dhaifu za umeme kutoka kwenye misuli ya ogani maalumu za umeme. Ili kutofautisha nyuga hizi na zile zilizotolewa na samaki wengine na mawindo yao, na jinsi mazingira yao ya karibu yanavyozipotosha, ngozi yao ina aina tatu za vidakaumeme. Udakaji wa umeme wanaowezesha hutumika katika uwindaji, utambuzi wa umeme na mawasiliano. Hata hivyo udakaji huu unahitaji usindikaji ngumu wa data katika saketi maalum ya neva kwa sababu inategemea uwezo wa kutofautisha kati ya nyuga za umeme zilizozalishwa binafsi na nyuga nyingine na kati ya sifa za nyuga zilizozalishwa binafsi na mabadiliko yao na mazingira. Ili kuwezesha usindikaji huu maalum wa data nakala ya kila utoaji wa chaji hufanywa kwa kulinganisha na uga wa umeme uonekanao inayoujenga. Ubongonyuma una jukumu muhimu katika usindikaji wa udakaji unaotegemea nakala hiyo. Maji yenye matope ambamo domodomo wanaishi yamesababisha kuwa udakaji wa umeme huo inajumuisha jukumu muhimu katika maisha yao na hii imesababisha ubongonyuma wao uwe mkubwa.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri- Gnathonemus longibarbis, Mputa Pua-ndefu
- Hippopotamyrus grahami, Mputa wa Graham
- Marcusenius devosi, Mputa wa Tana
- Marcusenius livingstonii, Mputa wa Livingston
- Marcusenius macrolepidotus, Mputa wa Rukwa, Mpuni au Nchemba
- Marcusenius nyasensis, Mputa wa Malawi, Nchemba au Ndaka
- Marcusenius rheni, Mputa wa Rhen
- Marcusenius stanleyanus, Mputa wa Tanganyika
- Marcusenius victoriae, Mputa wa Ziwa Victoria
- Mormyrops anguilloides, Linjolo
- Mormyrus bernhardi, Domodomo wa Bernhard
- Mormyrus caschive, Domodomo Pua-chupa
- Mormyrus hildebrandti, Domodomo wa Hildebrandt
- Mormyrus kannume, Domodomo wa Uganda au Mbete
- Mormyrus longirostris, Domodomo Pua-ndefu au Mbelewele
- Mormyrus macrocephalus, Domodomo Kichwa-kikubwa
- Mormyrus niloticus, Domodomo wa Naili
- Mormyrus tenuirostris, Domodomo wa Mto Athi
- Pollimyrus castelnaui, Mputa Kibete
- Pollimyrus nigricans, Mputa Mweusi
- Pollimyrus petherici, Mputa wa Khartumi
Picha
hariri-
Boulengeromyrus knoepffleri
-
Brienomyrus longianalis
-
Campylomormyrus curvirostris
-
Campylomormyrus elephas
-
Campyliomormyrus numenius
-
Campylomormyrus phantasticus
-
Campylomormyrus rhynchophorus
-
Campylomormyrus tamandua
-
Cyphomyrus psittacus
-
Hippopotamyrus castor
-
Ivindomyrus marchei
-
Marcusenius moorii
-
Linjolo (Mormyrops anguilloides)
-
Mbete (Mormyrus kannume)
-
Stomatorhinus walkeri
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
haririDomodomo kwenye hifadhidata ya samaki Archived 2 Oktoba 2018 at the Wayback Machine.