Horatius
(Elekezwa kutoka Horace)
Quintus Horatius Flaccus (pia: Horasi; 8 Desemba 65 KK - 27 Novemba 8 KK) alikuwa mshairi mashuhuri wa Roma ya Kale.
Alizaliwa kama mtoto wa mtumwa aliyepewa uhuru na bwana wake na kutajirika baadaye. Hivyo aliweza kumpa mwanawe elimu nzuri. Alisomea Roma na baadaye Ugiriki.
Aliandika mengi kwa lugha ya Kilatini akasifiwa wakati wake na katika karne zilizofuata.
Kati ya maneno yake yaliyorudiwa mara kwa mara ni:
- Sapere aude! - "Thubutu kujua" (yaani: Ujiamini kutumia akili!)
- Dulce et decorum est pro patria mori - "Ni tamu, tena inafaa, kufa kwa nchi yako."
- Carpe diem - "Shika siku" (yaani: Usipoteze fursa za kufurahia leo!)
Viungo vya nje
hariri- Espace Horace
- The works of Horace at The Latin Library
- Selected Poems of Horace
- The Perseus Project -- Latin and Greek authors (with English translations), including Horace
- Biography and chronology Archived 6 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
- Litweb Archived 14 Aprili 2006 at the Wayback Machine.
- Horace's works: text, concordances and frequency list