Ignas wa Laconi

(Elekezwa kutoka Ignasi wa Laconi)

Ignas wa Laconi, O.F.M. Cap. ni jina la kitawa la Vincenzo Peis (1701 - 11 Mei 1781) alikuwa bruda ombaomba wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka kijiji cha Laconi, mkoani Sardinia, (leo nchini Italia).

Sanamu yake iliyosimamishwa katikati ya Laconi.
Kanisa la Laconi alipopokea sakramenti za kuingizwa katika Ukristo.

Katika mitaa ya Cagliari na hata katika vilabu vya bandarini aliomba asichoke misaada kwa ajili ya watu fukara.

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri mwaka 1940, halafu mtakatifu mwaka 1951.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.