Isauri, Inosenti na wenzao

Isauri, Inosenti na wenzao Felisi, Ermia, Pelegrino na Bazili (walifariki Pojani, Makedonia, katika Albania ya leo) walikuwa Wakristo waliouawa kutokana na imani yao wakati wa dhuluma ya Dola la Roma.

Isauri alikuwa shemasi wa Athene (Ugiriki) aliyeondoka pamoja na Bazili ili wakashike maisha ya kitawa pangoni. Njiani walifuatwa na Felisi, Ermia na Pelegrino ambao waliuza mali yao na kuwapa maskini.

Lakini wazazi wao hawakupenda, hivyo waliposhindwa kuwarudisha waliwashtaki hata wakauawa kwa kukatwa kichwa [1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini[2].

Sikukuu yao ni tarehe 17 Juni[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.